Install REHOPOS on your device for lightning-fast access, distraction-free full-screen mode, and seamless everyday POS operations.
Fanya mauzo kwa sekunde chache, dhibiti stoo na tuma risiti za WhatsApp au Bluetooth kwa wateja moja kwa moja kutoka kwenye simu yako ya mkononi.
Una akaunti tayari? Ingia hapa
Unachagua bidhaa kwa kugusa kioo cha simu, unapokea malipo taslimu au ya simu, na stoo inapungua kiotomatiki.
Tofauti ya wazi kati ya kutumia madaftari ya mikono na kuendesha biashara yako kidigitali kupitia REHOPOS.
Mfumo mwepesi unaoeleweka haraka kwa mfanyabiashara na mfanyakazi yeyote.
Fanya mauzo kwa kugusa kioo cha simu yako au kuscan barcode. Inafaa simu za Android, iPhone, Tablet au kompyuta.
Fuatilia idadi halisi ya bidhaa zilizopo stoo na upate tahadhari mapema kabla mzigo haujaisha au muda wake haujapita.
Rekodi madeni ya wateja na kiasi walicholipa. Watumie vikumbusho vya heshima kwa njia ya WhatsApp au SMS bila usumbufu.
Chapa risiti kwa printa ndogo ya mfukoni ya Bluetooth (58mm/80mm) au mtumie mteja risiti rasmi kupitia WhatsApp bila karatasi.
Dakika chache tu kuanzisha duka lako na kuanza kufanya mauzo.
Andika jina la duka lako na namba ya simu. Akaunti yako inakuwa tayari mara moja.
Weka majina na bei za bidhaa zako kwa simu au pakia orodha yako yote kwa pamoja kupitia Excel.
Fanya mauzo kwa haraka na uwape wateja risiti safi za karatasi au kupitia WhatsApp papo hapo.
Hakuna gharama za siri wala ada za ufungaji. Chagua kifurushi kinachoendana na biashara yako.
Inafaa duka au biashara inayokua kwa kasi.
Inafaa duka au biashara inayokua kwa kasi.
Majibu ya moja kwa moja kuhusu mfumo wa REHOPOS.